LIVE MUDA HUU: ITAZAME MECHI YA YANGA 🆚 SINGIDA BS LIVE HAPA
Leo ndio siku ya mwisho kufunga hesabu za msimu wa mashindano 2024/25 kwa mchezo wa fainali kombe la CRDB kati ya Yanga dhidi ya Singida Black Stars ukipigwa katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar Mechi nyingine kubwa na aina yake itashuhudiwa visiwani Zanzibar siku nne tu baada ya mchezo wa dabi ya Kariakoo ulioamua ubingwa wa ligi kuu Yanga ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Simba na kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo Hii itakuwa fainali ya tano mfululizo kwa Yanga katika michuano hiyo, Wananchi wakilisaka taji la nne mfululizo Hata hivyo ni wazi haitakuwa mechi nyepesi, msimu huu Singida BS wamejipambanua kuwa timu imara wakifanikiwa kutinga fainali kwa kuiondoa Simba kwa ushindi wa mabao 3-1 katika hatua ya nusu fainali Yanga na Singida BS zinakutana kwa mara ya tatu msimu huu Yanga ikipata ushindi mwembamba katika mechi mbili zilizopita ambazo zote zilikuwa za ligi Mchezo unaokumbukwa zaidi ni ule wa duru ya kwanza ambao ulipigwa uwanja wa New Amaan Complex, Yanga ik...